Adhabu ya Joka
Bitugi Matundura, Worldreader
language
(Longhorn Publishers and Worldreader, Feb. 15, 2017)
Furaha ya kila mwanandoa huwa ni kupata mtoto… Kibuka na Kalimuzo wanaishi kwa miaka kumi na miwili bila kujaaliwa kupata mtoto. Maadamu Mungu si Athumani, hatimaye wanajaaliwa kupata mtoto wa kiume wanayemwita Ziro. Je, mtoto huyu alikuwa chanzo cha furaha au huzuni kwa wazazi wake? Hii ni hadithi ya kuwaonya vijana dhidi ya uhalifu kama vile wizi kwani Ziro anapata adhabu ya joka anapoiba sanduku lililodhaniwa kuwa na pesa nyingi sana.