Bitugi Matundura, Worldreader
Adha ya Kisauni
language
(Longhorn Publishers and Worldreader Feb. 15, 2017)
Hali ya usalama katika kijiji cha Kisauni ilikuwa imezorota sana. Wenyeji walihitajika kuwa nyumbani kwao saa kumi na moja unusu jioni na hawakuondoka humo kabla ya saa moja asubuhi. Kadhia za uhalifu zilizoanza kuchipuka katika kijiji hiki ndizo zinazovuruga na kutikisa utando wa amani na hatimaye udugu ukayeyuka na kuisha kabisa. Hii ni hadithi ya kuonya vijana kwamba magenge ya uhalifu hayafai kabisa katika jamii. Ni kweli kwamba uhalifu haulipi chochote!